Chama cha CHAWAKITA kinajishirikisha katika kushiriki makongamano mbali mbali yanayohusu kiswahili ili kujifunza mambo mengi.
CHAWAKITASUZA imepata nafasi ya kushiriki katika kongamano la kuwaaga wahitimu wa chuo cha mwalim Nyerere ambapo, mwenyekiti CHAWAKITA TAIFA na viongozi mbali mbali kutoka katika matawi tofauti.
Mgeni rasmi alikuwa ni OTHMAN BONERA.
Amesisitiza zaidi kwenye matumizi ya kiswahili na kuipa hadhi lugha ya kiswahili.
KONGAMANO LA CHAWAKITA-SUZA KUWAAGA WAHITIMU NA VIONGOZI WANAOMALIZA MUDA WAO.
KAULI MBIU YETU NI KISWAHILI NI CHACHU YA MAENDELEO YA MUAFRIKA.
KATIKA SHAMRA SHAMRA ZA KUKARIBISHA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI
MH: JUMA CHUM
MRAJIS WA BARAZA LA SANAA
Alitoa tamko kuwa CHAWAKITASUZA ITAKUWA NI CHAMA AMBACHO KITAJUULIKANA KISHERIA NA ITAKUWA HATUA YA KWANZA CHAMA HICHO KUPATA NGUVU ZAIDI.
Mh: Juma Chum. ameahidi kabla ya kufanyika Kongamano linalofuata la kuwakaribisha wanafunzi wapya na kuwaaga wahitimu waliopo atajitahidi kutatua changamoto kubwa ambazo zinakikabili chama chetu. tunamshukuru kwa mh. mrajis kwani ametupa muelekeo na matumaini ya kukiendeleza chama katika tawi la Suza. Pia hivi sasa chama kimesajiliwa rasmi katika baraza la sanaa zanzibar kwa shughuli mbali mbali za kudumisha utamaduni.
Tunaamini kuwa mafanikio yatakuja kwa uwezo wa Mungu na jitihada za viongozi katika kila hatua.
TUNAOMBA WANACHAMA WAZIDI KUKIPAISHA CHAMA KWA KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU NA VIONGOZI KATIKA FURSA ZITAKAZOJITOKEZA.
AFISA HABARI NA MAHUSIANO
CHAWAKITASUZA 🔥
twaha216@gmail.com
Kiswahili ndio CHACHU YA MAENDELEO YA MUAFRIKA.
KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI.
tarehe 13/11/2022.
CHAWAKITA katika matawi yaliopo Zanzibar wameandaa kongamano maalum kwaajili ya kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani, ambapo maadhimisho hayo yamefanyika MATEMWE katika ukumbi wa TUMAINI.
Mwenyeji wa eneo Hilo amefurahishwa sana na ujio huo kwani anakiri kuwa ni Kwa mara ya kwanza kufanyika Kwa kongamano Hilo toka kuadhimishwa Kwa SIKU ya kiswahili duniani.
CHAWAKITA KATIKA MATAWI YA
KUMBU KUMBU YA MWALIMU NYERERE TAWI LA KARUME
CHUO CHA ABDUL-RAHMAN AL- SUMEIT
NA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR SUZA
Ndio washiriki wa kongamano Hilo.
Aidha, viongozi katika matawi hayo wametoa shukrani zao za dhati kabisa kwa wale wote ambao wameshiriki kwa namna moja au nyengine katika kufanikisha jambo Hilo. Mungu awasimamie katika mambo yao yote.
SHEREHE YA KUWAKARIBISHA MWAKA WA KWANZA KTIKA CHAMA CHA CHAWAKITA-SUZA
Chama chetu kina kawaida ya kuandaa sherehe kila awamu kwaajili ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wanaojiunga na chawakita.
Siku ya jumamosi ya tarehe 12/11/2022 saa mbili asubuhi
wageni waliotarajiwa kuwasili ni
mgeni rasmi: Bi Saade Said Mbarouk. mwenyekiti wa BAKIZA
Mrajis wa baraza la Sanaa, sensa na utamaduni. MH: Juma Chum
Aisha Ali salum: Msoma risala katika sherehe akieleza mipango kazi ya chama, jitihada zinazochukuliwa na viongozi pamoja na changamoto zinazokikabili chama.
CHAWAKITA-SUZA 🔥 Umepata nafasi ya kushiriki katika baraza la Sanaa ndani ya wiki ya pili baada ya sherehe.
Ambae pia ni Afisa habari CHAWAKITA KATIKA NGAZI YA TAIFA.
Ametia saini mswada wa MH: mrajis katika utatuzi wa changamoto za chama.
KONGAMANO LA BARAZA LA KISWAHILI LA ZANZIBAR (BAKIZA).
CHAWAKITA-SUZA NA TAIFA KWA UJUMLA TUMEPATA NAFASI YA KUSHIRIKI KONGAMANO HILO.












Maoni
Chapisha Maoni