HISTORIA YA CHAWAKITA
CHAWAKITA ni chama Cha Wanafunzi na Wahitimu wa Kiswahili Vyuo vikuu na vya kati Tanzania kilichchozaliwa ni CHAWAKAMA, Chama Cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo Vikuu Afrika Mashariki kilicho anzishw 2004.
Mwaka 2006 SUZA ilijiunga rasmin na chama hicho na kuwa manachama halali ikishiriki kwenye makongamano na warsha mbali mbali ikiwemo kongamano la Kitaifa lilofanyika Burundi n.k.
Kutokana na mahitaji ya Kiserikali , Chama hiki kilisajiliwa na kanda ya Tanzania kwa jina la CHAWAKITA na kupata usajili wake 2019.
Chama hichi kinaendeshwa na Wanafunzi kutoka katika vyuo mbali mbali katika ngazi za kitaifa na kwenye matawi . Kwa sasa , Mwenyekiti wa CHAWKITA Tifa anatokea Chuo cha Abdul rahman Alsumeit.Ttaratibu za ubadilishwaji wa uongozi hufanyika kila baada ya mwaka mmoja katika ngazi za matawi na Taifa kwa mujibu ya katiba ya chama.
Tunashkuru mpaka sasa tunapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa uongozi wa Chuo chetu, walimu wetu pamoj na walezi wetu katika kukiendeleza chama hichi.
Tangu awali chama hichi kinaandaa kazi mbali mbali za kifasihi zinazotungwa na wanachama wetu wa chawakita. wanafunzi hujituma kadri ya uwezo wao kuonesha vipaji vyao huku wakiendelea kukuza chama na kukitangaza kiswahili.
Pia wanachama kupitia chawakita wanapata nafasi ya kushiriki tunzo mbali mbali za ndani na nje ya Afrika zinazohusu kiswahili.

Maoni
Chapisha Maoni